Skip to content

Month: April 2020

Matawi Ya Isimu.

Isimu-ubongo– ni tawi la isimu linalochunguza mahusiano kati ya lugha na michakato ya kiakili (ubongo), uzalishaji wa matamshi katika ujifunzaji wa lugha. Msingi mkubwa katika tawi hili la isimu ni kuwa mchakato wa uzungumzaji huanzia katika akili ya mtu. Hivyo mwanaisimu ubongo hujaribu kutafitina kueleza ni nini hasa kinatokea katika ubongo ambacho kinamwezesha mwanadamu kuzungumza. Pia hutafiti na kueleza matatizo katika lugha yanayotokana na matatizo katika ubongo wa mwanadamu. Isimujamii – Isimu Jamii (social linguistcs) – ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na… Read more Matawi Ya Isimu.

Sajili Ya Simu.

Hii ni lugha inayotumiwa katika mazungumzo ya simu. Sifa za lugha ya simu Mazungumzo ya simu ni mafupi, hutumia sentensi fupi zenye muundo rahisi. Hoja hutajwa moja kwa moja bila maneno mengi kwani ili kudhibiti gharama ya simu Huwa na kukatizana kwa maneno kati ya wazugumzaji. Huwa ni mazungumzo baina ya watu wawili pekee; anayepiga na anayepokea. Hutumia istilahi maalum za lugha ya simu kama neno ‘hello’ Huchanganya ndimi (kutumia maneno yasiyo ya lugha nyinginezo) ili kuwasilisha ujumbe kwa upesi. Ni lugha ya kujibizana.

Isimujamii.

Isimujamii– ni tawi la isimu (elimu ya lugha) linalochunguza namna lugha inavyotumika katika jamii na uhusiano baina yake. Tawi hili huzingatia matumizi ya lugha katika mazingira tofauti; aina mbali mbali za lugha na mazingira yake; uhusiano kati ya lugha na utamaduni wa jamii inayoitumia. Istilahi za isimujamii Isimu – ni mtalaa ambao huchunguza, huchanganua na pia kuchambua na kufafanua lugha kama mfumo wa mawasiliano baina ya wanadamu. Lugha – ni chombo cha mawasiliano baina ya watu. Lugha huzingatia mpangilio maalum wa sauti, maneno na sentensi. Sajili – ni mukhtadha/rejista mbalimbali… Read more Isimujamii.