Skip to content

Month: March 2020

Shairi la ukaraguni.

Tumekosa Nini? Mungu muumba dunia, mimea na wanadamu, Nimekuja nikilia, pasi kujali kaumu, Wewe ndiwe waridhia, pita nasi hali ngumu, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Kamwe uwezo hatuna, tungeishika dunia, Tuweze kutakasana, mawele sijeingia, Na hongo tungepeana, hasa kwa korona pia, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Yarabi tumejifunga, kwa vyumba pasi kutoka, Hata na hewa kupunga, mekuwa shida hakika, Halafu kutangatanga, pia imezuilika, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini. Au wafundisha nini, tuweze kulifahamu, Magoti tupige chini, kwa toba situhukumu, Tughofire kwa yakini, kwa korona loharamu, Mbona tunaangamia, Mungu tumekosa nini.… Read more Shairi la ukaraguni.

Aina Za Wadudu.

Funza/Tekenya-Huyu ni mdudu anayefafana sana na kiroboto na ambaye hupenya ngozini na kutaga mayai. Nzige-Mdudu ambaye husafiri masafa marefu na ambaye huharibu mimea kwa wingi. Tandu-Mdudu mwenye miguu mingi na ambaye huuma na ana sumu. Nondo-Mdudu anayefanya na kipepeo na hupenda kuruka usiku. Mbu-Mdudu ambaye hufyonza damu na kuuma watu na ambaye huhusika katika uambukizaji wa ugonjwa wa malaria. Mbungo-Mdudu mkubwa kuliko nzi, hufyonza damu na huhusika katika uambukizaji wa maradhi ya malale. Kiroboto-Mdudu ambaye huishi mwilini mwa mbwa,paka na hata wanyama wengine. Nyenze-Mdudu ambaye hutoa sauti kali usiku na… Read more Aina Za Wadudu.

Vipengele Vya Fani Katika Fasihi.

Mambo muhimu tunayohitaji kuzingatia tukiangazia fani ni kama yafuatayo. Mtindo-Huu ni utaratibu maalum ambao mtunzi wa kazi wa fasihi amefuata kujenga kazi yake.Hutofautiana katika hali ya mtunzi na mtunzi. Wahusika-Huweza kujumuisha watu, wanyama na viumbe vingine hai na hata mizimwi.Huwakilisha tabia maalum katika jamii. Mazingira/Mandhari-Hapa ndipo mahali ambapo matukio yote ya fasihi hutendeka.Huweza kuwa mazingira halisi au ya kubuni. Matumizi ya lugha-Ni mpangilio wa maneno, tamathali za semi kwa ufundi kulingana na mahitaji ya kazi yao. Muundo-Hii ni sura nzima ya kazi ya fasihi.

Fani za Lugha Katika Fasihi.

Ni ufundi wa uteuzi wa maneno katika kupamba lugha inayovutia hisia mseto kwa msomaji/hadhira. Aina ya fani za lugha zinazotumika katika fasihi ni kama zifuatazo. Utohozi-Hii ni mbinu ya uswahilishaji wa maneno yasiyo ya Kiswahili kuwa ya Kiswahili.K.m Bicycle-Baisikeli Kuchanganya ndimi-Hii ni mbinu ya kutumia maneno yasiyo ya Kiswahili katika sentensi ya Kiswahili.Nitaenda supermaket kesho asubuhi. Maswali ya Balagha-Hii ni mbinu ya kuuliza maswali yasiyo na majibu ili kusisitiza jambo. Methali-Hii ni mbinu ya kutumia misemo ya hekima yenye maana fiche.K.m Bura yangu sibadili na rehani. Taswira-Hii ni mbinu ya… Read more Fani za Lugha Katika Fasihi.