Usemi Taarifa.

Huu ni usemi unaotumika kueleza yale yaliyosemwa na mzungumzaji/msemaji bila ya kunukuu maneno yake moja kwa moja.Yafuatayo ni vipengele muhimu vya kuzingatia unaposhughulikia usemi huu:

  • Alama Za Uakifishaji kama vile alama ya hisi, alama ya kunukuu na alama ya kiulizi haitumiki kamwe.
  • Nafsi ya kwanza na ya pili hubadilika kuwa ya tatu.K.m “Mimi nitakuja kesho”,baba alisema.Baba alisema kuwa yeye atakuwa siku itakayofuatia.
  • Leo hubadilika kuwa siku hiyo.K.m “Nitaenda sokoni kesho”, mfanyabiashara alisema.Mfanyabiashara alisema kuwa angeenda sokoni siku itakayofuata.
  • Jana huwa siku iliyotangulia.”Tulisafiri jana,”wanafunzi walisema.Wanafunzi walisema kuwa walisafiri siku iliyotangulia.
  • Wakati ujao ‘Ta’ hubadilika na kuwa ‘Nge’.K.m “Tutawasili Kisumu kesho,”abiria walisema.Abiria walisema kuwa wangewasili Kisumu siku itakayofuata.
  • Kiambishi cha masharti ‘Ki’ pia hubadilika na kuwa ‘Nge’.K.m “Ukikimbia kwa kasi,utafika utepeni wa kwanza,”kocha alimshauri mwanariadha.Kocha alimshauri mwanariadha kuwa iwapo angekimbia kwa kasi angefika utepeni wa kwanza.
  • Sasa hubadilika na kuwa wakati ule/huo.”Nitakuja sasa hivi,”shangazi alisema.Shangazi alisema kuwa angekuja wakati ule.
  • Kwa kuwa alama ya hisi haitumiki maneno yanayohusiana na mshangao hutumika.”Kujeni hapa,”polisi alisema.Polisi aliwaamrisha waje pahala alipo.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s