Sifa kuu Bainifu za Lugha za Wanadamu.

Sifa zinazotofautisha lugha ya mwanadamu na mfumo wa mawasiliano wa wanyama ni:Unasifu,utabaka,uhamisho na uzalishaji.

Unasibu katika lugha ya mwanadamu ni ile hali ambapo sauti fulani zinawakilisha maana fulani katika jamii.Hata zile sauti zinazoingiza mlio wa Sauti nazo pia hukaribia tu ile sauti halisi inayowakilisha (onomatopea). Mengi ya maneno ni sehemu tu ya sauti inayotumika kama ishara inayowakilisha maana ya yale yaliyokusudiwa.Muundo sarufi wa lugha vilevile ni wa kinasibu kwani hakuna muundo wa aina moja mfano wa kirai au kishazi ambao kila lugha hauna budi kuufuata.

Utabaka ni ile hali ya lugha kuwa ni muunganiko wa vipande zinazounda lugha.Sauti zinaunda silabi,silabi zinajenga neno la kifonolojia,maneno yanakuwa virai.Kwa upande mwingine sarufi,mofimu inaunda shina na maneno, maneno yanakuwa virai,virai navyo vinakuwa vishazi, vishazi hatimaye inakuwa sentensi.Hata kwa upande wa semantiki wa chini wa vijenzi kujenga ule wa juu zaidi.

Uhamisho ni sifa ya kipekee ya lugha za binadamu.Mwanadamu anaweza kuongea Jambo ambalo halipo machoni mwao.K.m kuongelea tukio,watu au kitendo kilichopita au kile kinachoweza kutokea.

Uzalishaji pia hupatikana katika lugha za wanadamu kwani wazungumzaji waweza kuongeza sentensi, vishazi na hata visawe kwa kutumia mfumo wa maneno ambao haujawahi kutolewa na mtu mwingine yeyote duniani.Bora tu aweze kujieleza kwa njia atakayo yeye na hadhira imuelewe.

#Chuo kikuu cha Huria,2005, Tanzania.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s