Skip to content

Month: January 2020

Konsonanti.

Hii ni aina ya sauti katika lugha ambayo wakati wa utamkaji hewa huzuiliwa katika sehemu mbalimbali kinywani au pia hewa huzuiliwa kidogo baada ya kupita koromeo. Aina hii ya sauti hutambuliwa kwa kuzingatia sifa zifuatazo: 1.Mahali pa kutamka. 2.Namna ya utamkaji. 3.Mtikisiko au kutotikisika kwa koromeo.

Tofauti kati ya Fonolojia na Fonetiki.

Licha ya kwamba taaluma ya fonolojia na fonetiki hukaribiana sana, kutegemeana na kukamilishana kwa kuwa zote huchunguza sauti, kuna tofauti kadhaa kama zifuatazo. 1.Uchunguzi wa kifonolojia huzingatia mfumo maalum wenye utaratibu fulani ilhali uchambuzi wa kifonetiki. 2.Uchambuzi wa kifonolojia huzionyesha zile sifa bainifu katika lugha mahususi.Kwa upande mwingine taaluma ya fonetiki huorodhesha sauti zote na kutoa ufafanuzi kiumakinifu zinazoonesha tofauti zote za kifonetiki katika foni. 3.Fonolojia huwa nyingi kama idadi ya lugha zilizopo duniani kama vile fonolojia ya kijaluo,kijerumani,kifaransa n.k.Fonetiki nayo huwa moja tu. 4.Fonolojia hushughulikia sifa za kiarudhi zilizo… Read more Tofauti kati ya Fonolojia na Fonetiki.

Dhana ya Fonolojia.

Fonolojia ni taaluma inayoshughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumika katika lugha fulani mahususi.Kiwango hiki cha lugha huchunguza uamilifu wa sauti mahususi zinazotumika katika lugha maalumu. Kipashio cha chini kabisa cha Fonolojia ni fonimu.Fonimu ni sauti anuwai zinazotumika kuunda maneno katika lugha ya kiswahili.Aidha , kipashio hiki hutumika kutofautisha maneno ya lugha.K.m hapa na haba. Dhima ya kwanza ya fonolojia ni kueleza na kufafanua mifanyiko mbalimbali ya kifonolojia mathalani namna sauti zinabadilika kutoka sauti moja hadi nyingine hasa tunapojenga maneno tofauti. Kazi ya pili ni kuonyesha sifa za kiarudhi katika… Read more Dhana ya Fonolojia.