Skip to content

Mwenye kupaka midomo.

Nauliza si utani,wala sizuwi fitina Naomba jibu wendani,lenye kina na maana Hii rangi midomoni,huwa ina ma’na gani? Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Mahaba mnatatiza,mabinti wa siku hizi Nyoyo mnatuumiza,kisi sasa hatuwezi Midomo mnashangaza,walahi mwatupa kazi Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Rangi hii midomoni,nyengine hasa ni sumu Haina raha jamani,mapenzi kukosa hamu Mwatunyanyasa wendani,kisha na kutudhulumu Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Majike mloolewa,lengo lenu huwa gani? Kikweli mwajiumbuwa,hamvutii jamani Na yule ulochumbiwa,kisi upigwaje hani? Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi? Dume fulani majuzi,lilisaka sidechiki Kapigwa kisi mjuzi,penzi na yake mikiki Kurudi nyumbani… Read more Mwenye kupaka midomo.

Rais Fungua nchi.

Kwa muda tumenyamaza,lakini tumerejea, Hata kama twajikaza,ni mengi tumepitia, Na nyumbani twajilaza,sadirini twaumia, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Korona imepungua,na sasa wangoja nini? Wananchi twashangaa,mikutano hadharani, Ninakusihi fungua,tusiumie mbeleni, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Twaona nazo siasa,wabunge watukanana, Hawaoni ni makosa,inafaa kuwakana, Hakuna wa kuwanasa,ukweli kuna korona? Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Kila siku twakereka,hatuna matumaini, Ukweli twalalaika,tukiwa huku nyumbani, Vipi tutasaidika,na shida hizi jamani? Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Mjini na vijijini,watoto wamepotea, Tuambie zako plani,za nchi kuifungua, Twangoja yako idhini,kwa muda ‘mevumilia, Rais fungua nchi,tumechoka na nyumbani. Na… Read more Rais Fungua nchi.

Mbona nisirudi.

Natamani nikarudi, siku zile zamani Ila tu imenibidi, uwezo sina sinani Nami ningejitahidi, pale ninapotamani Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Natamani zama zile, zisokuwa na potole Lipopiga ukelele, nihudumiwe wavyele Ya kesho nisiyaole, vya shubiri nisivile Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Mambo ya kukosa kazi, katu nisiyaelewe Kodi ikawe upuzi, nisikie kwa wenyewe Sinao hata mchuzi, nyumba nje kafungiwe Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma? # Lakini ningejipanga, kuyafanya maamuzi Singekuwa tena bunga, nikashinde kwa upuzi Kuovu singejiunga, ningeenda na wajuzi Ila sasa nifanyeje, jua litarudi… Read more Mbona nisirudi.

Nani aliwaroga.

NANI AMEWAROGA? Lipokuja divolusheni, kadhani sluhu mepata, Usilojua Jamani, ni usiku wa matata, Kura liwapigieni, gavana na maseneta, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Meoza moja samaki, mtungo u mashakani, Wananchi wamehamaki, magavana chunguzeni, Mafisadi Kawasaki, pesa zetu okoeni, Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Sonko kumi milioni, taachama kwa Korane, Mia mbili milioni, zi mfukoni mwa Korane, Wakifika kortini, dhamana si Mara nne , Hivi leo twauliza, ni nani amewaroga? Ni makubwa ya Obado, ligawa na familiya, Mehukumiwa Obado, ila pesa mesaliya, Twalalamika si bado, pesa kuturudishiya, Hivi leo… Read more Nani aliwaroga.